Leo
July 14 2016 Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Frederick
Sumaye amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kanda ya Pwani, Sumaye ana wapinzani
wawili ambao ni John Gugunita na Gango Kidera, akizungumza baada ya
kurejesha Sumaye amesema……
>>>’wanachama
mbalimbali na viongozi kutoka kanda hii walifika nyumbani kwangu kama
mara tatu na baadae tukakutana sehemu nyingine wakiniomba nigombee
nafasi hii na wamenishwishi nimekubali na baadae jana wakasema wao ndio
watakaoniletea fomu, nikaijaza na leo nimeirudisha’
Nafasi zingine za uongozi ambazo zipo
wazi ni makamu mwenyekiti ambapo watu watatu wamejitokeza kugombea
nafasi hiyo akiwemo Saed Kubenea, nafasi ya mwekahazina wagombea watatu
wamejitokeza akiwemo aliyekuwa naibu waziri wa kazi na ajira wa serikali
ya awamu ya nne, Makongoro Mahanga.
0 comments:
Post a Comment