Tanzania
bado inaendelea kufanya vizuri kimataifa ambapo hivi karibuni iliingia
kwenye headlines ya Mtanzania Seleman Kitenge kutunukiwa tuzo na Crans
Forum vienna (Austria).
Seleman
anaingia kwenye list ya kuwa mtanzania wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo
zilizoanzishwa tangu mwaka 2010 ambapo atapata fursa ya kushiriki
mikutano mbalimbali ya kimataifa.
Sasa
Mtanzania huyu alikutana na Ayo TV na kueleza sababu zilizompelekea
kutunukiwa tuzo hiyo ni kutokana na ushiriki wake wa mijadala mbalimbali
ya kimaendeleo katika nchi za Russsia, Moroco na Azerbaijan, ndipo
wadau wakapendekeza jina lake katika tuzo hizo pia ametoa wito kwa
vijana wengine na kusema………
>>>‘Napenda kutoa wito kwa vijana wenzangu kuwa na uvumilivu na kuwa na moyo kujitolea katika programu mbalimbali za kulisaidia Taifa kama alivyosema katibu wa umoja wa mataifa kuwa hakuna jambo linatuhusu sisi bila sisi vijana’- Kitenge
0 comments:
Post a Comment